Events

MAFUNZO YA KAMATI ZA UFUATILIAJI WA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA (PETS)

Shirika la Tanzania Women for Self Initiative (TAWSEI) latoa mafunzo kwa kamati za ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma (PETS) juu ya umuhimu wa ufuatiliaji kupitia ushiriki na ushirikishwaji pamoja na mbinu za uibuaji wa miradi kuanzia ngazi za vitongoji kwa kutumia mbinu ya fursa na vikwazo iliyoboreshwa (O&OD), Kamati hizo za kutoka vijiji vya MARAMBA “B”, MATEMBONI na MBAMBAKOFI vinavyopatikana Kata ya Maramba, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga zimelishukuru shirika la TAWSEI kwa kuwapa mafunzo haya ambayo wanaamini watayatumia vyema ili kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao. Aidha mafunzo haya yaliyofanyika katika ukumbi wa JKT Maramba yalifunguliwa na Diwani wa Kata ya Maramba Mh. Peter Shemandia na kufungwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Maramba Bi Anastazia Tuni.

READ MORE
News

ENEO LA JENGO LA KUHIFADHIA MAITI.

TAWSEI, Bodi ya Afya ya kituo cha afya Maramba, viongozi wa serikali za vijiji vya Kata ya Maramba pamoja na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kikao cha uundwaji wa kamati zitakazosimamia ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti wakikagua eneo litakalotumika kujenga jengo hilo.

READ MORE
Events

USHAWISHI MARAMBA

Kutokana na changamoto ya ukosefu wa jengo la kuhifadhia maiti katika Kata ya Maramba, baadhi ya wananchi walijitokeza kwenye mafunzo ya ushawishi na uhamasishaji ili kujengewa uwezo wa kwenda kuelimishana na kuhimizana umuhim wa kuwepo kwa jengo hilo na upatikanaji rahisi wa huduma hiyo.

READ MORE