MAFUNZO YA KAMATI ZA UFUATILIAJI WA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA (PETS)
Shirika la Tanzania Women for Self Initiative (TAWSEI) latoa mafunzo kwa kamati za ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma (PETS) juu ya umuhimu wa ufuatiliaji kupitia ushiriki na ushirikishwaji pamoja na mbinu za uibuaji wa miradi kuanzia ngazi za vitongoji kwa kutumia mbinu ya fursa na vikwazo iliyoboreshwa (O&OD), Kamati hizo za kutoka vijiji vya MARAMBA “B”, MATEMBONI na MBAMBAKOFI vinavyopatikana Kata ya Maramba, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga zimelishukuru shirika la TAWSEI kwa kuwapa mafunzo haya ambayo wanaamini watayatumia vyema ili kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao. Aidha mafunzo haya yaliyofanyika katika ukumbi wa JKT Maramba yalifunguliwa na Diwani wa Kata ya Maramba Mh. Peter Shemandia na kufungwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Maramba Bi Anastazia Tuni.

